Uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura Dar es Salaam

Tume ya Taifa ya uchaguzi inawatangazia wananchi wote kuwa uhakiki wa Daftari la Awali la Kudumu la wapiga kura Mkoa wa Dar es Salaam unaanza Kesho tarehe 20/08/2015 katika baadhi ya Kata.

Hii ni kutokana na Mkoa huo kuwa wa Mwisho katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari na hivyo kuwa na muda mfupi wa Uchakataji wa taarifa katika kanzi data ya Tume.

zoezi hilo litaendelea hadi kata zote zitakapokamilika kuweka wazi Daftari hilo.

Wananchi mnaombwa kuangalia katika Magazeti orodha ya kata ambazo zimeanza zoezi hilo na zitakaofuatia baada ya hizi za awali.

Ifuatayo ni orodha ya kata na vituo ambavyo zoezi la Uwekaji wazi wa Daftari la awali umeanza ilala, kinondoni, temeke