Kuzialika Taasisi na Asasi zitakazotoa Elimu ya Mpiga KuraJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIATUME YA
TAIFA YA UCHAGUZI


KUZIALIKA
TAASISI NA ASASI ZITAKAZOTOA ELIMU

YA MPIGA KURA


Kifungu cha 4C cha
Sheria ya Uchaguzi, Sura 343 kinaipa mamlaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa
Elimu ya Mpiga Kura nchi nzima, kuratibu na kusimamia Taasisi/Asasi na watu
wanaotaka kutoa Elimu hiyo.


Kwa kuzingatia matakwa
ya Kifungu hicho, Tume imeanza kutoa Elimu ya Mpiga Kura nchi nzima kipindi
chote cha mwaka mzima.

Kwa mantiki hiyo, Tume inapenda
kuzialika Taasisi/Asasi zenye nia ya kutoa Elimu
ya
Mpiga Kura kuwasilisha maombi
yao Tume ya Taifa ya Uchaguzi kabla ya Tarehe 01 Februari, 2017.


Taasisi/Asasi
itayakayowasilisha maombi inatakiwa kukidhi vigezo vifuatavyo:-

1. Iwe na usajili kwa mujibu wa Sheria
za Tanzania.

2. Iwe imefanya kazi Tanzania si chini
ya miezi 6 toka kusajiliwa kwake.

3. Miongoni mwa Watendaji wake Wakuu
watatu, wawili wanapaswa wawe Watanzania.

4. Iwe haina taarifa za kuvuruga amani au
kuchochea fujo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na katika nchi yoyote.

5. Iwe tayari kujigharamia katika kutoa
Elimu ya Mpiga Kura.

Aidha, maombi hayo
yanatakiwa kuambatanishwa na:-

1. Cheti cha Usajili.

2. Katiba ya Taasisi /Asasi.

3. Majina ya Viongozi wa juu wa Taasisi/Asasi

4. Anuani kamili ya makazi (Physical
Address) na Namba za simu za Ofisini na Viongozi.

5. Zana za Elimu ya Mpiga Kura
(Vijarida, Vipeperushi, Mabango, Vipindi vilivyorekodiwa, T-shirt n.k.).

6. Ratiba itakayoonyesha tarehe na
mahali watakakotoa Elimu ya Mpiga Kura katika Halmashauri husika.

Tume inapenda kusisitiza
kwa Taasisi/Asasi kuwa Tume haihusiki na utolewaji wa Fedha kugharamia shughuli
za kutoa Elimu ya Mpiga Kura.

Tume itafuatilia
Taasisi/Asasi zitakazopewa Kibali cha kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa lengo la
kuona kama Elimu hiyo inatolewa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.


Maombi yote yatumwe kwa anuani
ifuatayo
:-

Mkurugenzi wa Uchaguzi,

Tume ya Taifa ya
Uchaguzi,

Jengo la Posta,

7 mtaa wa Ghana,

S.L.P 10923,

11300 DAR ES SALAAM.

TANGAZO
HILI LIMETOLEWA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI