Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Dimani, Zanzibar na Madiwani katika Kata 20 za Tanzania Bara, Januari 22, 2017

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA DIMANI - ZANZIBAR NA MADIWANI KATIKA
KATA ISHIRINI (20) KWENYE HALMASHAURI KUMI NA TISA (19) ZA TANZANIA BARA TAREHE
22 JANUARI, 2017

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia
wananchi wote wa Jimbo la Dimani, Wilaya ya Magharibi “B”, Mkoa wa Mjini
Magharibi – Zanzibar na Kata Ishirini (20) katika Halmashauri Kumi na Tisa (19)
za Tanzania Bara kuwa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge wa Jimbo hilo na Madiwani katika
Kata hizo utafanyika siku ya Jumapili tarehe 22/01/2017. Kata hizo na
Halmashauri na Mikoa kwenye mabano ni Ngarenanyuki (Meru DC, Arusha), Igombavanu
na Ikweha (Mufindi DC, Iringa), Kiwanja cha Ndege (Morogoro MC, Morogoro), Ihumwa
(Dodoma MC, Dodoma), Kijichi (Temeke MC, Dar es Salaam), Kahumulwa (Sengerema
DC, Mwanza) Maguu (Mbinga DC, Ruvuma), Ng’hambi (Mpwapwa DC, Dodoma), Kimwani (Muleba
DC, Kagera), Kinampundu (Mkalama DC, Singida), Isagehe (Kahama TC, Shinyanga),
Kasansa (Mpimbwe DC, Katavi), Duru (Babati DC, Manyara), Malya (Kwimba D.C, Mwanza), Misugusugu
(Kibaha TC, Pwani), Mateves (Arusha D.C, Arusha), Nkome (Geita DC, Geita),
Lembeni (Mwanga DC, Kilimanjaro) na Tanga (Songea MC, Ruvuma) na utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:-

1. SIKU: Wananchi watapiga Kura siku ya Jumapili tarehe
22/01/2017


2. VITUO: Zoezi la Upigaji Kura litafanyika
katika vituo vilivyotumika katika Uchaguzi Mkuu


uliofanyika tarehe 25/10/2015.


3. MUDA: Vituo vitafunguliwa saa 1:00 Asubuhi na
kufungwa saa 10:00 Jioni

1.
Watakaohusika
katika upigaji Kura ni wale walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura na wana kadi zao.

2.
Mpiga
Kura anatakiwa kwenda kwenye kituo cha kupigia Kura akiwa na Kadi yake ya
kupigia kura

3.
Mpiga
Kura anatakiwa kupanga mstari akiwa kituoni na kusubiri hadi zamu yake ya
kupiga kura itakapowadia. Watu wanye Ulemavu, Wagonjwa, Wajawazito, Akina Mama
wanaonyonyesha na Wazee watapata kipaumbele na hawahitajiki kupanga mstari

4.
Mpiga
Kura anatakiwa afuate maelekezo yote atakayopewa na Msimamizi wa Kituo muda
wote akiwa Kituoni.Kailima,
R. K


MKURUGENZI
WA UCHAGUZI

Tangazo Hili Limetolewa na Tume ya
Taifa ya Uchaguzi S. L. P 10932 Dar Es Salaam, Tel.+255 22 2114963-6. Nukushi:
+255 22 2113382. Barua Pepe: info@nec.go.tz.
Tovuti: www.nec.go.tz.