Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ina majukumu yafuatayo:

(a) Kusimamia na Kuendesha Uandikishaji wa Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(b) Kusimamia na Kuendesha Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(c) Kupitia na Kugawa Mipaka ya Jamhuri ya Muungano katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi wa Wabunge.

(d) Kusimamia na Kuendesha Uandikishaji wa Wapiga Kura na kuendesha Uchaguzi wa Madiwani Tanzania Bara.

(e) Kutangaza matokeo ya Viti Maalum vya wanawake vya Ubunge na Udiwani. ;

(f) Kutoa Elimu ya Mpiga Kura na kusimamia Watu na Asasi zitakazohusika katika Kutoa Elimu hiyo.

(g) Kutekeleza Majukumu mengine yatokanayo na Sheria itakayotungwa na Bunge.• Uchaguzi wa Rais
• Uchaguzi wa Wabunge
• Uchaguzi wa Madiwani Tanzania Bara

• Mfumo wa Uandikishaji Wapiga Kura wa hapo awali (OMR) ulionekana kupitwa na wakati na hivyo kuwa vigumu katika uhifadhi wa taarifa zake.
• Taarifa za kimaumbile (Bio metric Features) zinazochukuliwa zinatumika katika kulinganisha taarifa za watu mbalimbali na hivyo kuzuia watu kuwepo mara mbili katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
• Kadi Imara ya Mpiga kura
• Ili kuweza kutimiza haki yako katika Kupiga Kura siku ya Kura ya Maoni na Uchaguzi.
• Kuweza kushiriki katika uongozi Nchi yako.
Raia yeyote wa Tanzania aliyetimiza Umri wa miaka 18 na kuendelea na yule atakayetimiza Umri wa Miaka 18 Oktoba 2015 anafaa kuandikishwa kuwa Mpiga Kura.
Kipindi cha Uandikishaji Wapiga Kura katika eneo lako kitatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Vyombo vya Habari , Radio, TV na Magazeti.
Katika kituo cha Uandikishaji Wapiga Kura kilichopo jirani na eneo unaloishi.
Hakuna Nyaraka zozote zinazohitajika wakati wa Uandikishaji, Ijapokuwa kwa wale Wapiga Kura wenye Vitambulisho vya Upigaji Kura wanatakiwa kumkabidhi Mwandikishaji Msaidizi kadi yake ili kurahisisha zoezi la Uandikishaji.
• Ikiwa ana Uraia wa Nchi nyingine yaani sio Raia wa Tanzania,
• Amehukumiwa kifungo cha zaidi ya Miezi Sita,
• Amehukumiwa kifo na Mahakama za Tanzania,
• Amethibitika kuwa hana Akili timamu.
Ni kosa la Jinai mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja, na ikitokea, mtu ataadhibiwa kulingana na Sheria za Uchaguzi.
Ndio, Mawakala wa Vyama vya Siasa vyenye Usajili wanaruhusiwa kuwa na mwangalizi mmoja kwa kila kituo cha Uandikishaji Wapiga kura .
Uteuzi ni sehemu ya Mchakato wa Uchaguzi,ambapo Mgombea anachaguliwa na chama chake kugombea nafasi katika Uchaguzi
Atatangazwa kama Mgombea asiye na Mpinzani na hivyo kuwa amechaguliwa.