• English
  • |
  • Maswali yaulizwayo Mara kwa Mara   |  
  • Staff Mail

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Uchaguzi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Wajumbe wa Tume
    • Dira na Dhima
    • Jinsi NEC Ilivyoanzishwa
  • Uchaguzi
    • Mifumo ya Uchaguzi
    • Mzunguko wa Uchaguzi
    • Uchaguzi Mkuu
    • Uchaguzi Mdogo
    • Matokeo ya Uchaguzi
    • Kura ya Maoni
  • Wapiga Kura
    • Vituo vya Uandikishaji
    • Takwimu za Wapiga Kura
    • Elimu ya Mpiga Kura
    • Uhakiki
  • Machapisho
    • Sheria za Uchaguzi
    • Kanuni za Uchaguzi
    • Ripoti
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Zabuni
    • Zabuni za Ndani
    • Zabuni za Kimataifa
  • Wasiliana Nasi

Tume yapongezwa kwa usimamizi na matumizi Bora ya rasilimali za Serikali

Imewekwa: December 14, 2017

Mhe. Muhagama ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora iliyoridhia Bunge lipitishe fedha kiasi cha shilingi bilioni 10 kuiwezesha Tume kufanya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini .

Akizungumza na watendaji na baadhi ya watumishi wa Tume amesema kuwa ameridhishwa na utendaji kazi wao na namna Tume ilivyojipanga kutekeleza jukumu la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuelekea uchaguzi ujao wa mwaka 2020 kwa kuwa na mpango Kazi, unaochambua na kubainisha mahitaji muhimu yanayotakiwa, lini na wapi ili kazi hiyo iweze kufanyika kwa umakini.

“ Naipongeza sana Tume kwa kuendelea kufanya vizuri , nimegundua kuwa imejipanga vizuri kutekeleza majukumu yake ambayo yameainishwa Katika Katiba, kwa niaba ya Waziri Mkuu nimekuja hapa na timu ya watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora walioridhia Bunge lipitishe fedha shilingi Bilioni 10 ili kuiwezesha kufanya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura” Amesema.

Mhe. Mhagama ameeleza kuwa kazi hiyo kazi ya utekelezaji wa maagizo hayo ya Bunge inazingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 5 kifungu kidogo cha 3 (a) ambacho kimeweka uanzishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini na Ibara ya 74 kifungu kidogo cha 6 (a) na (e) ambacho kinaipa Tume madaraka ya kuchukua jukumu la kuandikisha wapiga Kura nchini Tanzania.

Aidha, ameongeza kuwa Sheria ya Uchaguzi kifungu cha 15 (3) kinaipa madaraka Tume ya Uchaguzi kutengeneza mfumo na utaratibu wa uandikishaji wa wapiga Kura nchini na uboreshaji wa daftari hilo mara mbili kati ya Uchaguzi mkuu mmoja na unaofuata.

“Tunaelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa hiyo ili tuzingatie takwa la Katiba na takwa la Sheria ya Uchaguzi ambayo inasimamiwa na Tume ni lazima sasa Serikali ione kwamba inaisaidia Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wote tunajua kuwa utendaji wake ni huru lakini Serikali tunaowajibu wa kuhakikisha kuwa Tume inafanya kazi yake vizuri” Amesisitiza.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ameipongeza uongozi wa Tume kwa kuonyesha mfano katika kuondoa mazoea katika utendaji kazi ikiwemo utunzaji wa mali na rasilimali za Serikali.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuijengea uwezo Tume kwa kuipatia rasilimali na vitendea kazi inavyohitaji ili iweze kutimiza majukumu yake kwa wakati.

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo amemshukuru viongozi hao kwa kuzitembelea ofisi za Tume kuangalia maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuishukuru Serikali kwa kutenga shilingi Bilioni 10 zitakazotumika kwa ajili ya uboreshaji huo.

Amesisitiza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imejipanga kulitekeleza jukumu hilo kikamilifu na inaendelea kufanya maandalizi mbalimbali yakiwemo ya kuzipitia Mashine za BVR zitakazotumika kuandikisha wapiga Kura , kupitia mifumo Sheria na kanuni za Uboreshaji, kupitia vifaa vilivyopo ili kupunguza mzigo wa kununua vifaa vipya wakati wa zoezi hilo.

Habari Mpya

  • Tume yajibu madai ya Chadema kuhusu Uchaguzi Mdogo wa Februari 17, 2018
    Jan 01, 1970
  • Siha wapiga kura kwa amani
    Jan 01, 1970
  • “Jitokezeni kupiga kura, mkimaliza mrudi nyumbani” Msimamizi Jimbo la Siha
    Jan 01, 1970

Nifanyaje?

  • Kujiandikisha Kupiga Kura
  • Kupiga Kura

Machapisho

  • Uchaguzi Mkuu wa 2015
  • Safu ya Menejimenti
  • Uchaguzi wa Madiwani Mwaka 1994
  • Uchagzi Mkuu wa Mwaka 1985
  • Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge wa Mwaka 1980

Mawasiliano yetu

  • Address : P.O.Box 10923, Dar es Salaam, Ghana and Ohio Street
  • Namba ya Simu : +255 22 2114963-6
  • Nukushi : +255 22 2116740, +255 22 2127075
  • Barua Pepe : uchaguzi@nec.go.tz
  • Tovuti : www.nec.go.tz

Linki za Haraka

  • Maktaba ya Tume
  • Majukumu ya Msingi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Bunge la Tanzania
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Msajili wa Vyama vya Siasa

Kuwa karibu nasi

Jiunge na orodha ya baruapepe zetu ili uhabarishwe na kupata notisi kuhusu taarifa zetu mpya

Tufuatilie

@2018 Tume ya Taifa ya Uchaguzi . Haki zote zimehifadhiwa

  • Ramani ya Tovuti
  • Wasiliana Nasi