Habari

​Watumishi Tume waadhimisha Sherehe za Meimosi mwaka 2017 jijini Dar es salaam.

Imewekwa: 2017-05-03 11:28:00

Watumishi Tume waadhimisha Sherehe za Meimosi mwaka 2017 jijini Dar es salaam.

Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wameungana na wafanyakazi wengine kote nchini kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani , Meimosi iliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Wakiongozwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani, wafanyakazi wa Tume walishiriki katika maandamano yaliyopita mbele ya mgeni rasmi Mhe. Margaret Sitta (MB) wakiwa na bango lenye ujumbe usemao “ Utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura ni Msingi wa Ujenzi wa Demokrasia . Jitokeze, Sikiliza, Soma, Uliza ili Uelewe”

Ujumbe uliokua kwenye bango ulilenga kutoa hamasa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika programu endelevu ya utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura kote nchini.

Aidha, watumishi wa Tume walipita mbele ya mgeni rasmi na wageni mbalimbali walioalikwa wakiwa kwenye gari la wazi kuonesha namna Upigaji Kura unavyofanyika katika vituo vya kupigia Kura siku ya Uchaguzi ukiwa ni ujumbe kwamba katika Tume katika kusimamia Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani nchini Tanzania inazingatia Sheria, Kanuni na taratibu na kwamba chaguzi zote huendeshwa kwa uwazi na Haki.