Kinga za Kikatiba

KINGA ZA KIKATIBA ZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Uhuru wa Tume ya Uchaguzi Umeelezwa vizuri katika Ibara ya 74(11) na (12)  ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

  1. Katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Tume ya Taifa ya Uchaguzi haitalazimika kufuata Maagizo ,Maelekezo au Amri kutoka katika Mamlaka yoyote ile ya Serikali ama chama     chochote cha siasa.
  2. Hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na nguvu ya kuhoji kitu chochote ama maamuzi yoyote yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kutekeleza majukumu yake kama ilivyoainishwa kikatiba.
  3. Katika kutekeleza Majukumu yake Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni taasisi Huru ya Serikali.