Majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (1977)Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imepewa  majukumu yafuatayo;

  1. Kusimamia na kuendesha Uandikishaji wa Wapiga Kura kwaajili ya Uchaguzi wa Urais, Ubunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  2. Kusimamia na kuendesha Uchaguzi wa Rais na Ubunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  3. Kupitia mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika majimbo mbali mbali ya Uchaguzi wa Ubunge.
  4. Kusimamia na kuendesha Uandikishaji wa Wapiga Kura na kuendesha Uchaguzi wa Madiwani .
  5. Kutangaza matokeo ya Viti Maalum vya wanawake vya Ubunge na Udiwani. ;
  6. Kutoa Elimu ya Mpiga Kura na kusimamia Watu na Asasi zitazokazohusika katika Kutoa Elimu hiyo.
  7. Kutekeleza Majukumu mengine yatokanayo na sheria itzkzyotungwa na Bunge.